Friday, February 15, 2013

OMG..........GOLDIE IS DEAD




MSHIRIKI  wa Big Brother Africa 2012 kutoka Nigeria, Goldie Harvey, amefariki dunia muda mfupi, baada ya kurejea jijini Lagos.


Goldie ambaye jina lake kamili ni Susan Oluwabimpe Harvey, alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi, lakini hakuna sababu zilizoelezwa kuhusiana na kifo chake.


Nyota huyo ambaye pia alikuwa mwanamuziki hodari nchini humo, alifariki katika Hospitali ya Victoria Island, Lagos.


Goldie alifikwa na mauti mufa mfupi, baada ya kurejea nyumbani Lagos akitokea Los Angeles, Marekani alipokwenda kwa ajili ya tuzo za Grammy.


Taarifa za mitandao ya kijamii nchini Nigeria, zimewekwa taarifa zake huku wadau wengi wakionyesha kushitushwa na kifo cha Goldie.


"Ni mshitko mkubwa napenda kuwataarifu kwamba Goldie amefariki usiku wa jana (juzi) muda mfupi baada ya kurejea Lagos kutoka Los Angeles. Mungu aiweke roho yake mahali pema,"ulisomeka ujumbe mmoja katika mtandao wa Twitter.


Goldie ni mshiriki wa saba kuiwakilisha Nigeria katika shindano ya Big Brother Africa ambapo alishika nafasi ya tatu.


Taarifa za awali, zilidokeza Goldie alivishwa pete ya uchumba na aliyekuwa mshiriki mwenzake kutoka Kenya, rapa Prezzo.

No comments:

Post a Comment