Thursday, January 10, 2013

SIMBA WENGINE HAOOO OMAN

KIKOSI chenye wachezaji tisa na Kocha Msaidizi wa timu ya Simba kinaondoka kesho kwenda Oman kwa kambi ya wiki mbili. 

Jana kikosi chenye wachezaji wanane na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mfaransa Patrick Liewig na Kocha Msaidizi Mganda Moses Basena waliondoka na kwenda nchini humo.

 Simba itatumia kambi hiyo kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa barani Africa.

Wachezaji wanaoondoka kesho ni William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Hassan Isihaka, Komabil Keita, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abdallah Seseme, Said Demla.

 Wao Uturuki sie Oman majibu dimbani katika mzunguko wa pili wa ligi, all the best watani wa jadi.
No comments:

Post a Comment