Friday, December 28, 2012

SAFARI YA YANGA UTURUKI YAIVA


TIMU ya Yanga inaondoka Jumapili ikiwa na kikosi chenye wachezaji 27 na viongozi saba kwenda Uturuki kwa kambi ya wiki mbili katika mji wa Antarya na kufikia katika Hotel ya Sueon Beach ambayo iko katika ufukwe wa bahari. Wachezaji watakaoambatana na timu hiyo ni Ali Mustapha 'Bartez' Said Mohamed na Yusuf Abdul, Geofrey Taita, Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Stephano Mwasika, Kevin Yondan na Nadir Haroub 'Canavaro'.

Wengine ni Twite Kabange, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, George Banda, Jerry Tegete, David Luhende, Rehani Kibindu na Simon Msuva.

Viongozi wa benchi la ufundi kuwa ni Kocha Mkuu Ernest Brandts, kocha msaidizi Fred Minziro, kocha wa makipa Razack Siwa, daktari Sufian Juma, Ofisa Utawala Hafidh Salehe, Ofisa Habari Baraka Kizuguto na Mohamed Nyenje Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Yanga imetumia zaidi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya kambi hiyo, All the best Yanga na sisi Simba twaenda Oman....




















































No comments:

Post a Comment